Pixabay
23 Feb 2021 Toleo la habari Haki na usimamizi wa mazingira

Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa linaitimisha kikao chake kwa kutoa wito wa kushughulikia masuala yanayoathiri mazingira kwa dharura

Nairobi, Februari 23, 2021 –Mawaziri wa mazingira na viongozi wengineo kutoka kwa mataifa zaidi ya 150 wamehitimisha mkutano ulioendeshwa siku mbili mtandaoni wa Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-5)  ambapo baraza hili lilitoa onyo kuwa tunaweza kukabiliwa na majonjwa mengine tandavu tusipobadilisha jinsi tunavyoshughulikia mazingira.

Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa hukutana baada ya kila miaka miwili ili kutoa kipaumbele kwa sera za mazingira ulimwenguni na kukuza sheria za kimataifa za mazingira; maamuzi na maazimio yaliyochukuliwa na Nchi Wanachama wakati wa mkutano huo. Pia hufafanua kazi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Kutokana na janga la korona, Nchi Wanachama zilikubaliana kuhusu mbinu inayotumia njia mbili za UNEA-5: kikao cha mtandaoni (22-23 February 2021) na mkutano wa ana kwa ana utakaotokea mwezi wa Februari mwaka wa 2022.

Kikao kilichohudhuriwa na maelfu ya washiriki mtandaoni, ikijumuisha wajumbe zaidi ya 1,500 kutoka katika Mataifa 153, Wanachama wa Umoja wa Mataifa na Mawaziri wa Mazingira zaidi ya 60, Mkutano wa Baraza hili - ambao ulipeperushwa moja kwa moja mtandaoni - pia kilikubaliana kuhusu vipengele muhimu vya kazi ya UNEP, kuanzisha maadhimisho ya miaka 50 ya UNEP na kujadiliana na viongozi ambapo Nchi Wanachama zilishughulikia jinsi ya kukuza ulimwengu dhabiti usio na mapendeleo baada ya janga la korona.

"Inazidi kudhihirika kuwa changamoto za mazingira ni sehemu ya safari iliyo mbele yetu. Mioto misituni, vimbunga, ongezeko la joto, baridi kali isiyo na kifani, majanga ya nzige, mafuriko na ukame, yamekuwa matukio ya kawaida kiwango kwamba hayazungumziwi mno na vyombo vya habari," Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema katika hotuba yake kwa Baraza hilo. "Hali hizi mbaya zinazoongezeka za hali ya hewa na hali ya tabianchi zinatoa onyo kwetu ili tushughulikie changamoto tatu kwa sayari zinazotishia maisha yetu ya siku zijazo kwa jumla: changamoto ya tabianchi, bayoanuai na mazingira, na tatizo la uchafuzi wa mazingira na taka."

Katika taarifa ya kisiasa kwa kichwa cha "Kutazamia kikao cha ana kwa ana cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kitakachorejea mwaka wa 2022 - Ujumbe kutoka kwa kikao cha mtandaoni cha UNEA-5, Nairobi Februari 22 – 23, 2021" iliyoidhinishwa mwishoni mwa kikao hicho, Nchi Wanachama zilithibitisha tena majukumu ya UNEP kama mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani na kutoa wito wa kuwa na ushirikiano zaidi wa kukabiliana na changamoto za mazingira duniani.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Baraza lilitamani "kuimarisha msaada wetu kwa Umoja wa Mataifa na ushirikiano wa makampuni mbalimbali za kimataifa na tunaamini kuwa hatua ya pamoja ni muhimu ili kukabiliana kikamilifu na changamoto duniani." Iliendelea kuonya kwamba "kulipo hapo awali afya na ustawi wa binadamu vinategemea mazingira na na masuluhisho kutoka kwa mazingira, na tunafahamu kuwa tutakabiliwa na hatari za mara kwa mara za magonjwa tandavu katika siku zijazo ikiwa tutadumisha mifumo yetu ya sasa isiyoendelevu  katika maingiliano yetu na mazingira. ”

Sveinung Rotevatn, Rais wa UNEA-5 na Waziri wa Norway wa Hali ya Hewa na Mazingira, aliunga mkono onyo hilo.

"Kila mtu aliyekusanyika katika kika cha Baraza la Mazingira leo ana wasiwasi mkubwa kuhusu jinsi ugonjwa mtandavu unavyosababisha changamoto mpya na mbaya zaidi kwa afya, kwa jamii, kwa uchumi na kwa mazingira, na kuzidisha zile zilizopo, kote ulimwenguni," aliambia waandishi wa habari siku ya kufunga UNEA -5.

"Tutashirikiana kutambua hatua ambazo zinaweza kutusaidia kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, kutunza bayoanuai, na kupunguza uchafuzi wa mazingira, kwa wakati mmoja," aliongezea.

Baraza lilikubaliana kuhusu Mkakati wa Mda, Programu ya Kufanyia Kazi na bajeti ya UNEP. Mkakati huo mpya - ambao utachukua UNEP tangu mwaka wa 2022 hadi mwaka 2025 - unaweka wazi wajibu wa UNEP wa kuwezesha utekelezaji wa ahadi za Ajenda ya 2030.

“Mkakati huo unahusu  kubadilisha jinsi UNEP inavyofanya kazi na kushirikiana na Nchi Wanachama, taasisi za UN, sekta binafsi, asasi za kiraia na makundi ya vijana, ili tusonge mbele kwa bidii, haraka, na imara zaidi," alisema Bi Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP . “Mkakati huu unahusu kutoa sayansi na ujuzi kwa serikali. Mkakati huu pia unahusu kushirikiana na jamii nzima - kuhamisha nje ya wizara za mazingira ili kuimarisha uchukuaji wa hatua. Mkakati huo unahusu  kubadilisha jinsi UNEP inavyofanya kazi na kushirikiana na Nchi Wanachama, taasisi za UN, sekta binafsi, asasi za kiraia na makundi ya vijana, ili tusonge mbele kwa bidii, haraka, na imara zaidi," alisema Bi Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP . “Mkakati huu unahusu kutoa sayansi na ujuzi kwa serikali. Mkakati huu pia unahusu kushirikiana na jamii nzima - kuhamisha nje ya wizara za mazingira ili kuimarisha uchukuaji wa hatua. ”

Katika hafla ijayo ya UNEP ya kuadhimisha miaka 50 katika mwaka wa 2022, Bi Andersen alikiri umuhimu wa kutafakari kuhusu yaliyopita na kutazamia siku zijazo.

"Kwa kweli, hatua zilizochukuliwa hadi sasa ili kutunza mazingira ni ushahidi tosha wa kazi ya UNEP," Rais Kenyatta alikiri. "UNEP imekuwa na athari ya kudumu kuhusu jinsi tunavyotunza mazingira, uoto wa asili na maisha yetu."

Wakati wa kuelekea mkutano wa baraza hilo, UNEP ilizindua ripoti kuu, kwa ushirikiano wa Katibu Mkuu wa UN António Guterres – Kufanya Amani na Mazingira - ambayo inatoa mwongozo kamili wa jinsi ya kutatua changamoto tatu za sayari za mabadiliko ya tabianchi, bayoanuai na uchafuzi wa mazingira. Matukio kadhaa pia yalifanyika kuunga mkono UNEA-5, pamoja na Mkutano wa Vijana Ulimwenguni, Jukwaa la Biashara la Sera ya Sayansi na uzinduzi wa Muungano wa Kimataifa wa Chumi Endelevu Zinazotumia Bidhaa Kikamilifu

 “Siku chache zilizopita zimekuwa za kutia moyo. Tuliona juhudi mpya ulimwenguni za kutumia rasilimali kikamilifu, uchumi unaotumia bidhaa zilizotumika kuunda bidha zingine. Wito wa kushinikiza kupunguzwa kwa uchafu kutoka kwa misitu. Serikali, wanasayansi na mashirika ya biashara yakaja pamoja kuangalia data kubwa kama zana ya kuleta mabadiliko. Vijana wanapaza sauti zao na kutuambia 'hakuna chochote kutuhusu, bila kutushirikisha' na kutoa wito kwa fedha zinazolengwa kuwezesha wao kushiriki zaidi, "Bi Andersen aliongezea.

 MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. 

Kuhusu Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa
Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa ni jukwaa la ngazi ya juu zaidi duniani linaloleta pamoka wakuu wa nchi, mawaziri wa mazingira, CEOs kampuni za kimataifa, NGOs, wanaharakati wa mazingira, na kadhalika ili kujadili ahadi za kimataifa kuhusiana na utunzaji wa mazingira.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa