UNEP / Stephanie Foote
31 Mar 2021 Tukio Matumizi bora ya rasilimali

Flipflopi inaonyesha umuhimu wa kukuza uchumi unaotumia bidhaa za plastiki zilizotumuka kuunda bidhaa zingine

UNEP / Stephanie Foote

Mara nyingi, katika majuma matatu yaliyopita, Flipflopi, mashua iliyotengenezwa kutoka kwa plastiki iliyotumika, ikijumuisha ndara kuukuu, imekua ikitua kwenye mabandari kwenye Ziwa Victoria. Kikosi kwenye chombo hicho kilicho na urefu wa mita 10 kinanuia kuhamasisha kuhusu plastiki inayohatarisha ziwa kubwa mno barani Afrika – na kuonnesha kuwa taka inaweza kutumika kuunda vitu vya thamani.

"Flipflopi iliundwa ili kuonyesha dunia kuwa kuna uwezekano wa kuunda vitu vya thamani kutoka kwa taka ya plastiki," alisema Ali Skanda, mwanzilishi mwenza wa Flipflopi.

Safari ya mashua hiyo inayodhaminiwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), inatokea wakati muhimu kwa Ziwa Victoria na kwa Kenya, amesema Llorenç Milà I Canals, msimamizi wa mradi wa UNEP wa Life Cycle Initiative.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na UNEP ulionyesha kuwa asilimia 27 ya taka ya plastiki nchini Kenya hukusanywa na kwa hiyo taka, ni asilimia 7 tu inayotumiwa kuunda bidhaa nchini Kenya.

Tatizo hii ni la kimataifa. Hali ya binadamu ya kuzalisha bidhaa za plastiki za bei nafuu, kuzitumia na hatimaye kuzitupa, ilimesababisha changamoto ya uchafuzi kote ulimwenguni na inahatarisha hali asilia ya dunia na maisha ya binadamu.

 "Ukikibali kuwa unaweza unaweza kuchimba rasilimali na kuitupa, na kuiuza kwa bei rahisi bila kugharamia mambo mengine, unatoa moja kwa moja ruzuku ya kuhatarisha mazingira, ”anasema Milà I Canals. "Tunapata vitu kwa bei nafuu mno, ila tunalipia tu nusu ya gharama yake. Na hali hii inaenda kuleta matatizo katika siku zijazo."

Kuchunguza upya mienendo yetu kuhusiana na plastiki

The multi-coloured deck of the Flipflopi dhow
Flipflopi iliundwa kutoka kwa taka ya plastiki ikijumuisha ndara, zilizotumiwa kuunda sehemu kubwa ya shehena na sehemu ya juu. Picha: UNEP / Stephanie Foote

Kwa kipindi cha miaka hamsini iliyopita, uzalishaji wa plastiki umeongezeka zaidi ya mara 22. Binadamu sasa huzalisha tani milioni 300 ya taka ya plastiki kila mwaka na tani milioni 8 hujipata baharini. Taka nyingi pia huingia kwenye vyanzo vya maji, kama vile Ziwa Victoria, linalopitia Tanzania, Uganda na Kenya. Mojawapo ya utafiti uliofanywa mwaka wa 2015 ulionyesha kuwa asilimia 20 ya samaki ziwani humo ilikuwa na chembechembe za plastiki, vipande vya taka visivyozidi milimita 5 kwa urefu. Hali hii inaweza kuwa na madhara ya kudumu kwa familia 200,000 za wavuvi wanaooishi karibu na Ziwa Victoria.

Kikosi cha Flipflopi, kinachofanya safari ya pili, kinakuza mtindo wa uchumi unaotumia bidhaa zaidi ya mara moja, unalenga kutumia bidhaa tena na kupunguza uharibifu. Chanzo kikuu cha uchafuzi wa plastiki ni kile wataalamu wanachosema ni mfumo wa matumizi wa "chukua-tumia-tupa", unaopelekea bidhaa kuundwa, kutumiwa kwa mda na kutupwa.

Kote ulimwenguni, uchumi unatumia bidhaa zilizotumiwa kuunda bidhaa zingine ni muhimu ili kupunguza uchafuzi na uzalishaji wa gesi ya ukaa. Iwapo bidhaa zitakarabatiwa na kuboreshwa, dunia inaweza kupunguza matumizi yake ya malighafi kwa asilimia 99, kwa mjibu wa ripoti ya UNEP ya International Resource Panel (Jopo la Kimataifa la Malighafi).

Huanza, kwa mjibu wa Milà I Canals, na kubuni bidhaa kutoka kwa taka ili kuwa bidhaa zinazoweza kutumika tena, na kupunguza athari kwa mazingira katika mchakato wa kutengeneza na kutupa.

"Tuna ahadi za kimataifa za kupiga hatua ya kupunguza kiwango cha taka ya plastiki," alisema. "Ila tunahitaji pia kuzingatia mito ili kupunguza kiwango cha plastiki katika uchumi,"

Kubuni ajira

Hata bidhaa za plastiki zinazotupwa ni njia ya kipato katika maeneo ambayo ukusanyaji wa plastiki ni sehemu kuu ya mapato kwa watu wanaofanya kazi za rejareja.

Mfano mzuri unatoka nchini Kenya, ambapo kampuni yenye usuli wake nchini humo, Mr. Green Trading, imeajiri zaidi ya watu 600 kukusanya na kutenga plastiki na polyesta. Kile kinachoweza kutumiwa tena hutumiwa kuunda vidude na kuuziwa makampuni kutimia kufunga bidhaa.

Juhudi ya kuunda bidhaa mpya kutoka kwa vitu vilivyotumika ni "njia ya kuwa na ajira isiyoisha kwa ambao wameshasahaulika,"  anasema mwanzilishi Keiran Smith, anayelenga hatimaye kuajiri waokota taka 4,000.

"Kama eneo kuu la uzalishaji wa plastiki katika eneo la Afrika Mashariki, Kenya inaweza kuwa mstari mbele kwenye ukusanyaji, ubadilishaji na uuzaji wa plastiki kupitia mfumo unaojitosheleza," alisema.

Kampuni nyingine zinaunda bidhaa kutoka kwa platiki iliyotumika ziko mstari mbele kuleta mabadiliko. Mbia wa Flipflopi, Wakfu wa Taka Taka  huelimisha watu kuhusu uchafuzi wa plastiki huku ikibuni nafasi za kazi na miundo msingi za kuwezesha kuunda bidhaa kutoka kwa plastiki iliyotumika.

Kushirikisha wenyeji

Two children hold a sign protesting plastic pollution
TKikosi cha Flipflopi  kinanuia kuhamasisha Wanaafrika Mashariki kuhusu ongezeko la plastiki kwenye Ziwa Victoria. Picha: Flipflopi

Kwa kubadilisha angalau sehemu ya uchumi uwe unaounda bidhaa kutoka kwa zile zilizotumika unaowezesha kuondoa taka ya plastiki kutoka kwa mazingira na kuunda bidhaa zingine, jamii za eneo la Ziwa Victoria zinaweza kuwa nguzo kuu ya mapinduzi ya viwanda visivyochafua mazingira.

Dipesh Pabari, mwanzilishi mwenza wa mradi wa Flipflopi na nahodha wa safari ya Ziwa Victoria, anasisitiza kuwa jamii za wenyeji zinapaswa kushirikishwa kwenye kutafuta masuluhisho ya kutumia bidhaa zilizotengenezwa kutoka kwa zingine iwezekanapo – ikijuisha kupenda na kutegemea ziwa hilo.

Ziwa Victoria ni mojawapo ya mifumo mikuu ya ekolijia ya maji safi na huwezesha maisha ya watu milioni 40, kwa kuwapa chakula na kipato.

 

Maudhui Yanayokaribiana