UNEP / Kibuuka Mukisa
10 Dec 2021 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Jinsi Daktari mmoja wa mifugo alivyoleta mabadiliko katika nyanja ya uhifadhi barani Afrika

UNEP / Kibuuka Mukisa

Huenda ikawa ni tumbili wa jirani aliyeshuka chini kujiunga naye alipokuwa anajifunza piano, au klabu ya wanyamapori aliyoanzisha katika shule ya msingi mjini Kampala, Uganda.  Lakini tangu akiwa mdogo sana, Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka, Bingwa wa Dunia kwenye kitengo cha Sayansi na Ubunifu mwaka huu, alifahamu kuwa alitaka kufanya kazi na wanyama.

 "Kimsingi, wanyama kipenzi walikuwa marafiki zangu wa kwanza," alisema Kalema-Zikusoka, daktari wa wanyamapori kwa kusomea ambaye ameendelea kwa miongo mitatu kusaidia kuwalinda baadhi ya wanyama wa familia ya sokwe walioadimu zaidi duniani, ikiwa ni pamoja na sokwe wa milimani walio hatarini kuangamia.  Nyingi ya kazi yake imekuwa katika jamii maskini za Afrika Mashariki ambazo zinapakana na maeneo ya hifadhi, ambapo amesaidia kuboresha huduma za afya na kuunda fursa za kujipatia fedha, na kufanya wenyeji wengi kuwa washirika wa kuhifadhi.

"Gladys Kalema-Zikusoka ni mwanzilishi wa uhifadhi wa wanyamapori unaoongozwa na jamii," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.  "Katika sehemu nyingi, matatizo ya kifedha yanaweza kusababisha migogoro kati ya wanadamu na wanyama. Lakini kazi yake imeonyesha jinsi mizozo inavyoweza kusuluhishwa jamii za wenyeji zikichukua usukani wa kutunza mazingira na wanyamapori wanaowazunguka, na hivyo kuleta manufaa kwa viumbe vyote.”

Akiungwa mkono na familia yake, Kalema-Zikusoka alianza safari yake ya elimu ya kimataifa, alipata shahada za digrii nchini Uganda, Uingereza na Marekani. Alipofikisha miaka 20 ikianza, alirejea nchini Uganda kwa mafunzo ya kazi, ambayo hatimaye ilikuwa nguzo ya kazi yake baadaye, Mbuga ya Kitaifa ya Bwindi Impenetrable iliyoko vijinini  maeneo maskini kusini magharibi mwa nchi.

Ilikuwa mwanzo wa utalii wa sokwe huko Bwindi na Kalema-Zikusoka, ambapo wakati huo alikuwa mwanafunzi mdogo wa udaktari wa mifugo, aligundua kuwa uhifadhi haikuwa kazi rahisi. "Kulikuwa na watu waliozingatia utalii na uhifadhi katika jamii," alikumbuka. "Kulikuwa na walinzi na askaripori na Peace Corps na mahali pa wageni kulala wakati nilipoondoka huko, nilielewa jinsi utalii na uhifadhi ulivyokuwa mgumu."

Kuna ukosefu wa uwakilishi wa wenyeji miongoni mwa wahifadhi. Tunahitaji mabingwa zaidi kutoka kwa wenyeji, kwa sababu hawa ndio watakaofanya uamuzi kwa niaba ya jamii na nchi zao.

Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka

 

Kalema-Zikusoka alikuwa daktari wa mifugo wa kwanza kabisa wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda. Huko, alianza kutumia mbinu mpya ya kufanya kazi kwa wanyamapori - ambayo ilijikita katika kuboresha maisha na mapato vijijini karibu na Bwindi.

“(Hiyo inawezesha) binadamu kufurahia maisha bora na kuwa na mwelekeo chanya zaidi kuhusu uhifadhi.  Unapowaonyesha watu kwamba unawajali na kujali afya na ustawi wao, unawasaidia kuishi vyema na wanyamapori.”

Hiyo ikawa kanuni iliyoongoza shirika ambalo Kalema-Zikusoka alianzisha takribani miaka 20 iliyopita:  Conservation Through Public Health. Limepanua kielelezo chake cha afya viijijini hadi maeneo yaliyohifadhiwa karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Virunga katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, pamoja na maeneo mawili yasiyohifadhiwa ya Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Elgon nchini Uganda. Mbali na kuhimiza usafi na mazoea bora ya usafi wa mazingira, kikosi hiki pia kinaunga mkono upangaji uzazi.

Kukubali kuna maingiliano kati ya wanadamu na wanyamapori, na kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama kati ya watu na wanyama, ilikuwa muhimu kwa Kalema-Zikusoka kwani alichukua wajibu mkuu wa kutoa mwongozo kwa serikali ya Uganda jinsi ya kukabiliana na janga la COVID-19.

A woman walking in a forest
Kalema-Zikusoka alikuwa daktari wa mifugo wa kwanza kabisa wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda. ​​Picha: UNEP/ Kibuuka Mukisa

Kuzuia watu kusafiri kote duniani kuliathiri sekta ya utalii kusini-magharibi mwa Uganda, na kulazimisha wengine kurudia kazi moja hatari: ujangili. Hilo lilitishia mafanikio makubwa yaliyofikiwa ya kuimarisha idadi ya sokwe wa milimani katika eneo la Bwindi, ambao idadi yao imeongezeka polepole hadi wamefikia zaidi ya 400. Hii inawakilisha karibu nusu ya idadi ya viumbe hao walio hatarini kuangamia ambao bado wanaishi porini. 

Conservation Through Public Health lilitoa mazao yanayokua haraka kwa familia, na kuwawezesha angalau kulima chakula cha kutosha kujilisha wenyewe.   Pia waliiachia jamii ujumbe muhimu.  "Tuliwaambia, lazima muendelee kulinda wanyamapori kwa sababu imewasaidia kiasi hiki.  Huu ndio mustakabali wenu.”

Mzozo kati ya watu na wanyama ni mojawapo ya vitishio vikuu kwa maisha ya muda mrefu ya baadhi ya viumbe vya kipekee zaidi duniani, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Mfuko wa Mazingira Duniani wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).  Katika nchi nyingi kama Uganda, mzozo huo, pamoja na hatari za kiafya za COVID-19 umehatarisha zaidi maisha ya viumbe vilivyo hatarini kuangamia.

Kalema-Zikusoka alifanya kazi na wafanyikazi wa mbuga za kitaifa kuhimiza wageni na askaripori kuvaa barakoa, sio tu kuzuia maambukizi ya COVID-19 kati yao wenyewe, lakini pia kutunza sokwe, ambao wanaweza kuambukizwa na vimelea vinavyoenezwa na binadamu.  Kazi hiyo inaweza kua na kuwa miongozo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama - maambukizi ambayo hutokea kati ya wanadamu na wanyama - na mafunzo kwa wafanyakazi wa afya wa eneo hilo ili kukabiliana na COVID-19.  Sasa mataifa 21 barani Afrika - ikiwa ni pamoja na nchi 13 ambazo zina idadi ya nyani wanaopungua - zimetia saini miongozo hiyo.

"Kwa kweli tunabadilisha kielelezo cha kuzuia ugonjwa kutoka kwa wanyama ili kuzuia COVID-19 kutegemea eneo," Kalema-Zikusoka alisema.  

A young gorilla in a forest
Kwa kipindi cha miongo kadhaa iliyopita, idadi ya sokwe wa milimani katika Mbuga ya Kitaifa ya Wanyama ya Bwindi Impenetrable imeongezeka polepole hadi wamefikia zaidi ya 400. Picha: UNEP / Kibuuka Mukisa

Conservation Through Public Health lilitoa mazao yanayokua haraka kwa familia, na kuwawezesha angalau kulima chakula cha kutosha kujilisha wenyewe.   Pia waliiachia jamii ujumbe muhimu.  "Tuliwaambia, lazima muendelee kulinda wanyamapori kwa sababu imewasaidia kiasi hiki.  Huu ndio mustakabali wenu.”

Anayetambulika duniani kote kwa kazi yake, Kalema-Zikusoka, anasema kuwa anatumai atawatia moyo vijana wa Kiafrika kuchagua kazi za uhifadhi. 

"Kuna ukosefu wa uwakilishi wa wenyeji miongoni mwa wahifadhi.  Sio wengi wanatoka sehemu ambazo kuna wanyama walio hatarini kuangamia hupatikana," alisema.  "Tunahitaji mabingwa zaidi kutoka kwa wenyeji, kwa sababu hawa ndio watakaofanya uamuzi kwa niaba ya jamii na nchi zao."

 

Matuzo ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa Mabingwa wa Dunia na Vijana Bingwa Duniani hutuzwa watu binafsi, makundi na mashirika ambayo juhudi zao huwa na mabadiliko chanya kwa mazingira. Tuzo linalotolewa kila mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la ngazi la UN linalotolewa kwa heshima ya mazingira.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza miaka ya kuanzia 2021 hadi 2030 kuwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia.  Muongo unaoongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), la Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano wa wabia, unalenga kuzuia, kusitisha, na kukukabiliana na uharibifu na kudidimia kwa mifumo ya ekolojia kote duniani. Unalenga kuboresha mabilioni ya hekta ya ardhi ya nchi kavu pamoja na mifumo ya ekolojia ya majini.  Wito wa kimataifa wa kuchukua hatua, Muongo wa Umoja wa Mataifa u

Tembelea www.decadeonrestoration.org ili kujifahamisha zaisi zaidi.