Asia ya Pasifiki ndilo eneo linalokua kwa kasi duniani. Pia ni eneo lenye tofauti kubwa sana wakati wa mlinganisho. Ni maskani kwa baadhi ya nchi ndogo sana na nchi maskini sana duniani na pia kwa nchi kubwa sana na nchi tajiri sana ulimwenguni. Ijapokuwa mamilioni ya watu wameokolewa kutokana na umaskini, eneo hilo linasalia kuwa maskani kwa takribani nusu ya watu maskini ulimwenguni.
Maendeleo yameambatana na changamoto. Miji inayoendelea kukua kwa kazi, maisha ya kiwango cha juu na ongozeko la watu wanaohitaji kutumia rasilimali na wanaohitaji huduma inawekea aridhi na maliasilia shinikizo kubwa katika eneo hilo. Hali hii inazua changamoto ya kupata maendeleo endelevu katika hili eneo. Kwa upande mwingine, nchi huungoza katika kubuni sera na mwelekeo wa kufuatwa. Mfano ni mpango wa Bhutan wa 'Bhutan’s Gross National Happiness', mpango wa Thailandi wa uchumi unaojiendeleza (Thailand’s sufficiency economy) na Mpango wa China wa kuwezesha maendeleo ya hali ya juu (quality growth model of China).
Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa hufanya kazi na nchi za Asia ya pasifiki ili kuleta maendeleo yanayowezesha kuwa na matumizi mazuri ya malighafi, kupunguza uharibifu wa mazingira na kuleta manufaa ya kijamii na ya kiuchumi kwa watu kutoka eneo hili. Sisi hutilia mkazo kupatikana kwa masuluhisho kwa changamoto zinazokabili mazingira kwa njia ya uvumbuzi na yenye manufaa katika eneo hili. Tunatumia mbinu inayotilia maanani vipengele vyote vitatu vya maendeleo endelevu - vya kiuchumi, vya kijamii na vya mazingira. Pia tunasaidia nchi kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.
Tunafanya kazi na halmashauri za kitaifa na za mitaa, mashirika ya uraia, mashirika ya Umoja wa Mataifa, taasisi za fedha, mashirika ya kikanda na mitandao ya kikanda, taasisi za utafiti na sekta za binafsi.