Kuendeleza Haki ya Kuwa na Mazingira Bora

Kuwezesha utunzaji wa mazingira kufikiwa na watu wengi 

Wajibu wa nyanja ya haki za binadamu zinazohusiana na mazingira safi, salama, bora na endelevu unakua. Vivyo hivyo, kutegemeana kwa haki za binadamu na mazingira kunakua kwa kasi kwa kukubalika na kueleweka miongoni mwa serikali.  Zaidi ya nchi 150 zina wajibu wa kisheria wa kuheshimu, kulinda na kutimiza haki ya kuwa na mazingira bora. Kuendeleza wajibu wa haki za binadamu zinazohusiana na mazingira hujengea uwezo watu binafsi, watu wote, na jamii wa kukabiliana na changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi.

Tarehe 8 Oktoba, Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kihistoria linalotambua kuwa mazingira safi, bora na endelevu ni haki ya binadamu. Azimio la Baraza la Haki za Binadamu ni wakati muhimu katika mapambano dhidi ya changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP Inger Andersen amelitaja azimio hili kuwa "hatua muhimu ya kujenga sayari kama makazi salama na ya haki kwa wote," na kuliita azimio hili "ngao kwa watu binafsi na jamii dhidi ya madhara kwa afya na maisha yao."  Soma taarifa kamili hapa.

UNEP inasaidia kutambua,kukuza na kutekeleza haki za binadamu zinazohusiana na mazingira kupitia mbinu inayozingatia mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupitia Mpango wa Haki za Mazingira, ambao ni mkusanyiko wa kazi zinazozingatia haki zinazofanywa na UNEP na washirika wake wanaojitolea kukuza, kulinda na kuheshimu majukumu ya haki za binadamu yanayohusiana na kufurahia mazingira salama, safi, bora na endelevu.
 

Haki za Mazingira ni zipi?

Haki zako za Mazingira ni zipi?

Watetezi wa Mazingira ni akina nani?

Soma Sera ya Umoja wa Mataifa ya Watetezi wa Mazingira