Pexels
16 Oct 2020 Toleo la habari Youth, education & environment

Tunajivunia vijana Waafrika wanaoleta mabadiliko kutokana na uchafuzi wa plastiki

Nairobi, Octoba 16, 2020 – Zaidi ya vijana Waafrika 400 walituzwa kwa kuwa mstari mbele kukabiliana na uchafuzi wa plastiki katika jamii zao kupitia shindano la Tide Turners Plastic. Katika shughuli hiyo ya kiwango cha juu, viongozi wa kisiasa, viongozi wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa na mwimbaji kutoka Ghana aliyependekezwa kushiriki katika tuzo la Grammy, Rocky Dawuni waliwapongeza vijana Waafrika walio mstari mbele kuleta mabadiliko kote duniani kwa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki.

Mkutano Mkuu wa Vijana kutoka Afrika –Shindano la Tide Turners Plastic Challenge linatambua umuhimu wa vijana zaidi ya 400 waliofaulu kukamilasha awamu zote tatu zaTide Turners Plastic Challenge Badge. Washiriki katika shindano hili wamedhihirisha kuwa wao ni viongozi kwa kuhamasisha watu kupitia mitandao ya kijamii, kuhimiza kuwepo na kampeni za ukusanyaji wa taka, na kuonesha kuwa uendelevu katika maisha yao na kadhalika.

Shindalo ambalo limefadhiliwa na uingereza kwa kipindi cha miaka miwili sasa, Tide Turners Plastic Challenge limewezesha vijana zaidi ya 225,000 kutoka katika nchi 25 ikijumuisha vijana 50,000 kutoka barani Afrika kushiriki. Shindano hilo linawezesha washiriki kujifunza kupitia viwango vitatu tofauti: mwanzo, kiongozi, na bingwa.

Vijana zaidi ya 1,500 walishiriki kwenye mkutano huo wa kiwango cha juu ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNEP) kwa ushirikiano na muungano wa Shirika la Skauti wa Kike DunianiShirika la Maskauti Duniani na Junior Achievement Afrika.

"Kama skauti wa kike mstaafu, ninajivunia Tide Turners na vijana wote wanaotutia moyo walioshiriki; kufikia sasa, zaidi ya vijana 50,000 kutoka katika nchi 18 kote ulimwenguni wamejiunga na programu hii. Tuendelee vivyo hivyo, kwa kuongeza nchi saba zaidi ili kuweza kufikia nusu ya nchi barani Afrika," alisema Joyce Msuya, Naibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP.

Mkutano uliojumuisha maskauti  wakati wa shughuli yao inayotokea kila mwaka ya Jamboree on the Air and Jamboree on the Internet event (JOTA-JOTI) ili kubadilishana maarifa kutokana na juhudi za vijana za kukabiliana na uchafuzi wa plastiki na kuwa msitari mbele kushughulikia mazingira katika jamii zao. Vijana sita waletamabadiliko walizungumzia visa vyao kuhusu jinsi walivyosababisha mabadiliko na kuwashawishi wenzao kujiunga nao ili kukabiliana na uchafuzi wa plastiki.

"Shindano la Tide Turners Plastic Challenge lilinipa fursa kuu ya kupitisha ujumbe wangu dhidi ya uchafu wa plastiki na kushiriki masuluhisho yangu," alisema Fyona Seesurrun, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22 kutoka Mauritius, mmoja wa mabingwa aliyetuzwa wakati wa mkutano huo.

"Mamalia 100,000 na ndegu milioni moja hufa kila mwaka kwa kula au kukwama ndani ya plastiki kila mwaka. Tusipofanya juhudi, kiwango cha idadi ya plastiki baharini kitaongezeka mara tatu kufikia mwaka wa 2025. Ni sharti tushirikiane kuzishughulikia sasa. Tide Turners ni kikosi cha kupigiwa mfano, kinachohimiza kizazi kipya cha viongozi kukabiliana na uchafuzi wa plastiki katika jamii zao. Hii ndiyo sababu inayopelekea Uingereza kusaidia UNEP kuimarisha kazi ya Tide Turners Plastic Challenge Badge kufikia nchi 20 zaidi kote ulimwenguni", alisema Zac Goldsmith, Waziri wa Uingereza wa Hali ya Pasifiki na Mazingira. 

Mwanamziki wa Ghana aliyependekezwa kuwania tuzo la Rocky Dawun – Balozi wa Nia Njema wa UNEP – pia alihutubia vijana wakati wa mkutano huo na kuwatumbuiza wageni kupitia nyimbo kama vile "Rock Your Soul".

Tide Turners Plastic Challenge Badge ni beji ya ya kwanza kutolewa kwa maskauti iliyotengenezwa kutoka kwa plastiki iliyotumika; shindano hili limejumuishwa kwenye jukwaa la kidijitali kwenye mradi wa kuelimisha maskauti kuhusu mazingira kote ulimwenguni. Earth Tribe, inayoleta pamoja maskauti milioni 54 kote ulimwenguni ni vuguvugu la vijana wanaopigania mazingira, na hutoa fursa kwa vijana kujifunza na kuchukua hatua za kushughulikia masuala nyeti ya mazingira yanayoathiri jamii zao.  

Katika mwaka wa 2021, waandalizi watajumuisha kipengele kipya kwenye beji na lengo la kushawishi kuwepo na mabadiliko ya kisera na mienendo.

Kila mwaka, zaidi ya tani milioni 8 za plastiki huingia baharini, na kuhatarisha maisha ya viumbe wa baharini, maeneo ya uvuvi, na utalii na hugharimu takribani dola bilioni 8 kugharamia hasara kwa mifumo ya ekolojia ya baharini. Uzalishaji wa bidhaa za plastiki duniani katika mwaka wa 2018 ulikadiriwa kuwa trilioni milioni 359 na kufikia mwaka wa 2040, kiwango cha plastiki katika bahari zetu kinaweza kuongezeka mara tatu zaidi.

MAKALA KWA WAHARIRI

Tide Turners Afrika, mwaka wa 2020 imefadhiliwa na Uingereza kwa ushirikiano na Vuguvugu la Muungano wa Maskaauti Duniani (WOSM), Shirika la Maskauti wa Kike Duniani (WAGGGS), Junior Achievement, shule, vyuo (vikuu) na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa.

Wabia wengine ni: Taasisi za serikali kama vile Mamlaka ya Kitaifa ya Kushughulikia Mazingira (NEMA) nchini Kenya, Centre Ivorian Anti-Pollution (CIAPOL), Shirika la Kusimamia Bahari na Usalama la Nigeria (NMASA), Shirika la Kushughulikia Mazingira nchini Sierra Leone, Shirika la Ghana National Plastic Action Partnership (NPAP) na Blue Action Network (BAN).

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP in mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Sam Barratt, Mkuu wa Vijana, Elimu na Uhamasishaji
Bryan Michuki, Msimamizi wa Mradi, Tide Turners