Athari za ongezeko la nyuzijoto 1.1 ziko hapa leo na zinaongezeka kwa kasi na hali ya matukio mabaya mno ya hali ya hewa kuanzia kwa mawimbi ya joto, ukame, mafuriko, dhoruba za msimu wa baridi, vimbunga na mioto ya mwituni. (IPCC)
- Joto la wastani ulimwenguni katika mwaka wa 2019 lilikuwa nyuzijoto 1.1, juu kuliko kipindi cha kabla ya viwanda, kwa mjibu wa WMO.
- 2019 ilihitimisha muongo wa joto la kipekee ulimwenguni, kupungua kwa barafu na usawa wa bahari kutokana na gesi za ukaa zinazozalishwa na shughuli za binadamu. (WMO)
- Asilimia 30 ya idadi ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na mawimbi mabaya ya joto yanayotokea zaidi ya siku 20 kwa mwaka. (Ukweli kuhusu Kupunguza Kiwango cha Joto na Mabadiliko ya Tabianchi, UNEP)
- Wastani wa joto kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2019) na kipindi cha miaka kumi (2010-2019) ndio ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa. (WMO)
- Mwaka wa 2019 ulichukua nafasi ya pili kwa kurekodi kiwango cha juu zaidi cha joto. (WMO)
- Katika mwaka wa 2019, jumla ya uzalishaji wa gesi ya ukaa, ikijumuisha mabadiliko ya matumizi ya ardhi, ilifikia kiwango kipya sawa na gigatani 59.1 za kabonidioksidi (GtCO2e). (EGR, 2020)
- Kwa kuzingatia ahadi ambazo hazitoshi kote ulimwenguni za kupunguza uzalishaji wa gezi zinazochafua mazingira, kuongezeka kwa gesi ya ukaa kutokana na jamii kurudi kutumia kaboni nyingi baada ya ugonjwa mtandavu unaweza kupelekea uzalishaji katika mwaka wa 2030 kuongezeka zaidi hadi GtCO2e 60. (EGR, 2020)