Hakuna utatuzi wa dharura ya tabianchi na matumizi ya kupindukia ya malighafi. Lakini iwapo binadamu watatunza, kushughulikia na kuboresha mazingira kwa njia endelevu, tunaweza kushughulikia changamoto katika jamii, kudumisha ustawi wa watu na kukuza manufa ya bayoanuai.
Kwa kushirikiana na mazingira kufanya kazi, uzalishaji wa hewa chafu unaweza kupunguzwa kwa gigatoni 11.7 za hewa ya ukaa kwa mwaka kufikia mwaka wa 2030, zaidi ya asilimia 40 ya kile kinachohitajika ili kupunguza ongezeko la joto duniani.
Takriban dola za Marekani bilioni 133 kwa mwaka kwa sasa hutumiwa kwa masuluhisho kutokana na mazingira, huku fedha za umma zikiwa ni asilimia 86 na fedha za kibinafsi zikiwa asilimia 14. Lakini hatua za dharura zaidi zinahitajika.
Ili kutumia uwezo kamili wa asili na kupelekea mafanikio ya Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia wa 2021-2030, uwekezaji mkubwa unahitajika katika kile ambacho mazingira hufanya vyema kabisa: kujiponya.
Mbinu inayotumiwa na UNEP kutekeleza masuluhisho yanayotokana na mazingira
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na washikadau mbalimbali – kuanzia na jamii ndogo nyanjani hadi kwa ngazi za juu za serikali – kubadilisha uhusiano wa binadamu na mazingira na kutoa masuluhisho endelevu kwa janga linalojitokeza la mabadiliko ya tabianchi.
UNEP, pamoja na Muungano wa Kimataifa wa Kuhifadhi Mazingira (IUCN) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), wanasimamia Muongo wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, ambao unalenga upanuzi wa matumizi ya mbinu za kilimo zinazojali ekolojia, upandaji miti mahahi imekatwa na upandaji miti, na kadhalika. UNEP pia huchangia kwa mipango ya upandaji miti na kilimo kinachojali mazingira. Programu hizi hupunguza uharibifu wa ardhi huku zikifyonza hewa ya ukaa na kusaidia kuhamasisha kusaidia bayoanuai.
UNEP inashirikiana na FAO na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kutekeleza Mpango wa UN-REDD wa kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutokana na uharibifu wa misitu. UNEP pia husaidia nchi kufafanua, kutekeleza na kufuatilia mipango yao ya kitaifa ya kushughulikia bayoanuai na kupanga kukabiliana janga la mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia mfumo wa ekolojia.
Nyenzo zaidi: