13 Oct 2020 Tukio Malengo ya Maendeleo Endelevu

Usipuuze mafunzo kutokana na Mdororo wa Uchumi: Ripoti mpya ya UNEP

 "Kwa sasa, dunia inapitia nyakati mbaya mno za kifedha na kiuchumi kuwahi kushudiwa kwenye historia. Changamoto hizi zimepelekea kubuni sera ambazo hazikutarajiwa ili kuzishughulikia: gharama ya hisa ilipungua mno, kiwango cha hata kufikia sufuri katika hali zinginezo, na mabilioni ya dola kutolewa kama hisa za mtaji na mtaji kwa benki kote duniani."

Umesikia kuhusu haya? Mtaalamu wa masuala ya uchumi, Ed Barbie alisema kati ya mwaka wa 2008 na mwaka wa 2009 dunia ilipokuwa inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi. Kipindi hicho, wataalamu walizitaka nchi kujumuisha ushughulikiaji wa mazingira kwa njia endelevu zitakapokuwa zinajiamarisha, ila nyingi hazikufanya hivyo.

Sasa, zaidi ya muongo mmoja baadaye, ripoti mpya kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) inasema kuwa dunia ina fursa ya pili - na inaweza kuwa ya mwisho - ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na changamoto zinginezo za mazingira. Ripoti iliyoandikwa na Barbier, profesa katika chuo kikuu cha America’s Colorado State University, inatoa mafunzo kutoka kwa Mdororo wa Uchumi (Great Recession) na kutoa wito kwa serikali kubuni mikakati dhabiti za kukubaliana na uharibifu wa mazingira zinapoimarisha uchumi baada ya COVID-19. Makala, Building a Greener Recovery: Lessons from the Great Recession, ni ya kwanza kwa mfululizo wa ripoti za UNEP zinazonuia kusaidia nchi kujiimarisha kwa njia endelevu baada ya ugonjwa mtandavu.

Makala haya yanasema kuwa wakati wa hali mbaya ya uchumi, kuna baadhi ya nchi zilizowekeza kwenye miradi inayotumia nishati kikamilifu, na nishati isiyochafua mazingira. Juhudi hizi zilibuni nafasi za kazi na kuimarisha matumizi ya nishati jadidifu kwa miaka kadhaa ila hazikutoa msaada wa kudumu ya kukabiliana na gesi ya ukaa katika chumi ulimwenguni.

Wakati huu, makala hayo yanatoa wito kwa serikali kuweka mikakati ya kati ya miaka 5 na miaka 10 kwa kufanya mabadiliko katika uwekezaji kwa umma na kwa sheria, ikijumuisha kuweka ushuru ili kufanya kuwa vigumu kusababisha uchafuzi. Yanasema hali hii itasaidia kuleta mabadiliko ili kuwa na uchumi usiochafua mazingira na kuwezesha kuimarisha uchumi kwa njia endelevu.

Makala haya pia yanapendekeza utaratibu mbalimbali wa kutunga sheria katika nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea. Kwa mataifa ya kipato cha chini na kipato cha kadri, yanayopitia changamoto za kifedha kutokana na janga, ripoti hiyo ilipendekeza:

  • kuacha kutumia nishati ya visukuku na kuanza kutumia nishati isiyochafua mazingira na kuimarisha upatikanaji wa nishati jadidifu katika maeneo ya mashambani; 
  • kupunguza gharama za vifaa za unyunyuziaji ili kuboresha miundo msingi ya usambasaji wa maji, ya usafi na ya maji taka; na 
  • kutekeleza “tropical carbon tax” ili kufadhili upandaji wa miti katika maeneo iliyokatwa na kuboresha mifumo ya ekolojia.

Dunia ina mengi ya kufanya kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa mjibu wa ripoti ya UNEP ya Emissions Gap. Iwapo hatua za kushughulikia mazingira zingechukuliwa kikamilifu tangu mwaka wa 2010, uzalishaji wa gesi chafu ungepungua duniani kwa asilimia 3.3 kwa mwaka na kuepuka ongezeko la joto kwa nyuzijoto 1.5 duniani, ambalo ni hatari kwa mazingira. Hata hivyo, kwa kuwa haya hayakufanyika, tutahitaji kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7.6 kwa mwaka.

Makala haya ya utafiti yalizinduliwa wakati wa kikao cha ufunguzi cha Mradi wa UNEP wa Fedha, kikao kinachotokea kila baada ya miaka miwili Global Roundtable.

 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: Laila Saada (laila.saada@un.org)