12 Aug 2020 Andikablogu Youth, education & environment

Umuhimu wa vijana wa Kiafrika katika majadiliano ya kimataifa kuhusu mazingira

Umuhimu wa vijana wa Kiafrika katika majadiliano ya kimataifa kuhusu mazingira

Kila mwaka, tarehe 12 Agosti ni  Siku ya Vijana Duniani, na kauli mbiu ya mwaka huu ni Shirikisha Vijana katika Juhudi za Kimataifa. Hapa, Sylvia Nagginda, Nnabagereka (Malkia) wa Buganda, Vanessa Nakate, mganda mhamasishaji wa masuala ya mazingira naMusonda Mumba, Msimamizi wa Kitengo cha Nchi Kavu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) wanazungumza kuhusu baadhi ya miradi inayowezesha vijana kusikizwa wakati wa kufanya maamuzi muhimu kuhusu mazingira.

Mwaka wa 2020 umefanya ulimwengu kuhangaishwa na ugonjwa mtandavu ambao haukutarajiwa huku kukiwa na uwezekano wa kutokea kwa majanga kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Athari zake zinaonekana barani Afrika, hasa kwa wanawake, watoto na vijana. Maeneo mengi barani Afrika yameathiriwa na majanga yanayotokana na hali ya hewa kama vile mafuriko na kiangazi, yanayoathiri maisha na kipato. 

Nchi changa mno duniani – kwa kuzingatia umri wa wastani wa watu wote – zinapatikana barani Afrika, kwa mjibu wa makadirio yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa ya Makadirio ya Idadi ya Watu Duniani Mwaka wa 2019. Wakfu wa Nnabageraka hujihusisha na kuwezesha vijana nchini Uganda kusikika katika masuala ya kimataifa.

Wakfu ulioanzishwa miaka 20 iliyopita, huongozwa na falsafa yaObuntubulamu (sawa na Ubuntu – “utu kwa wenzetu”). Unahimiza vijana kujiona kama jamii nzima wala sio watu binafsi, huwafunza kushirikiana na jamii, kuhusu masuala ya mazingira na masuala ya uchumi, ili kuwawezesha kuwa wapiganiaji wa maendeleo endelevu. Wakfu huo hushirikiana na UNEP na Taasisi za Umoja wa Mataifa. 

UN inapoadhumisha miaka 75 mwaka huu, na huku tukiwa tumesalia tu na miezi inayopungua minne kufika mwaka wa 2021, wakati tunapoingia muongo wa mwisho wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ni wakati mwafaka wa vijana Waafrika kuzungumza, kuhamasisha na kuchukua hatua. Vijana barani Afrika tayari wanafanya ubunifu muhimu na kutumia teknolojia isiyokuwa na madhara mabaya mno.

Vijana Waafrika wanasikika pia katika michakato ya kimataifa, hasa kuhusiana na mabadiliko ya tabiachi.  Wakati Muongo wa UN wa Uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia (2021-2030) unapoanza katika mwaka wa 2021, Vijana Waafrika waliulizwa kutoa maoni yao kwa kina. Kufikia mwaka wa 2030, wengi wa vijana hawa watashiriki katika michakato ya kufanya maamuzi katika nchi zao na hata kuvuka mipaka.    

Ni katika muongo huu ndiposa wabia wa UNEP, Mtandao wa Wanawake Wanamazingira wa Kiafrika (NAWE) walipozindua kampeni ya 'Guardians4Earth and Landscape Guardian’s Campaign' mnano Aprili, mwaka wa 2020. Kampeni hii inawaleta pamoja wanawake na wanaume kutoka pembe zote za dunia ili kufanya kazi kama 'walinzi' wa mandhari yao, na kusaidia katika uboreshaji wake katika muongo ujao (2021-2030). NAWE huunganisha Mkufunzi wa Mandhari (aliye na elimu ya kiufundi ya kutosha) na walinzi hao ili kuwaelimisha na kuwaongeza ujuzi

Mmoja wa Wakufunzi wa Mandhari nchini Uganda ni kijana mwanaharakati wa mazingira Vanessa Nakate.  Vanessa ahamasishi tu nchini Uganda, pia yeye huzungumza kuhusu masuala nyeti ya mazingira katika Congo Basin, eneo lililo na idadi ya zaidi ya Waafrika milioni 40. Kama wengi wa vijana wenzake, yuko tayari kushiriki katika mchakato wa kufanya uamuzi katika masuala haya nyeti.  

Tunapoelekea muongo wa mwisho wa maendeleo endelevu, tunatoa maoni yafuatayo kwa waunda sera na kwa vijana barani Afrika, ili waweze kushirikianakufanya kazi ili kuwa na mustakabali mwema kwa mazingira:

  1. Shiriki: Viongozi/waunda sera na vijana wanahitaji kushiriki katika ngazi ya jamii, ambapo hatua nyingi zinahitaji kuchuliwa. Vijana Waafrika hawawezi kuendelea kuwa watazamaji wa hatima yao wenyewe. 
  2. Kuwepo:  Viongozi na vijana wanahitaji kuwepo na kuelewa kuwa masuala kama vile mabadiliko ya tabianchi huathiri WOTE moja kwa moja au vinginevyo. 
  3. Sikiliza: Ni vyema pande zote mbili kufanya mazoezi ya kusikiliza ili kuleta mshikamano na kuchukua hatua katika jamii, hasa kuhusiana na uboreshaji. 
  4. Juhudi zetu ni muhimu: Janga hili linatukumbusha kuwa juhudi nyanjani zinategemea mno Waafrika wenyewe, bali siyo misaada wala kusaidiwa na wengine.  Mali halisi ya maarifa barani imekuwa ikipokezwa kutoka kizazi hadi kizazi na huwa hasa ya kisayansi. Tufanye maamuzi kwa kutegemea maarifa na ujuzi uliopo.
  5. Kuna uwezekano wa ajira zisizochafua mazingira:  Idadi ya viongozi na vijana barani Afrika waaokuza na kuboresha uchumi kwa kutumia bidhaa tena na tena inaongezeka-kwa kuchukulia mazingira kama chanzo cha ajira na kama kiteka uchumi.  Sera za kuunga mkono kazi zisizochafua mazingira ni shariti ziwe na mashiko na kujumuisha vijana. 

Kutokana na hekima ya Nnabagereka – "Tunapokosa mwelekeo kuhusu sisi ni kina nani kwa kutojiambia ukweli, kuwa wakarimu na wenye utu– hatuwezi kushughulikia na kutunza Dunia."

Tunatoa wito kwa vijana wa waunda sera barani Afrika kujali mazingira kama sehemu ya maadili muhimu. Kuhifadhi, kutunza na kuboresha mazingira tunamoishi kutahakikisha nasi ia tunaishi vizuri na kufurahia maisha.